Friday

YAJUE MADHARA YA SODA KWA AFYA YAKO!

  

Sina shaka wengi wetu hatukuwa tunajua madhara yasababishwayo na unywaji wa soda kiburudisho kinachopendwa na wengi.Lakini leo kupitia blog hii ya grace kyasi utapata kujuzika juu ya madhara yatokanayo na unywaji wa kinywaji hiki aina ya soda pale tu inaponywewa zaidi ya mara moja kwa siku au mara kwa mara;
    
   Kutokana na utafiti uliofanywa kwa kina na watafiti wa masuala ya vyakula na vinywaji nchini Marekani inaonesha kuwa Soda inauwezo mkubwa wa kuhatarisha figo za binadamu.Hatahivyo utafiti huo uliofanywa na watafiti kutoka chuo kikuu cha Harvard kilichopo nchini Marekani kwa zaidi ya wanawake 3000 nchini humo na kugundua kuwa unywaji wa soda unawaongezea hatari mara mbili ya kudhurika na figo.

   Watafiti hao wameeleza kuwa matatizo hayo ya figo huweza kuwapata wanawake mara wanapokunywa soda zaidi ya mbili kwa siku,ambapo figo huanza kushuka utendaji kazi wake wa kawaida kitu ambacho kinaweza kusababisha madhara makubwa kiafya.Mbali na soda watafiti hao pia wamevituhumu vyakula vyenye sukari kuwa ndivyo husababisha matatizo ya Figo na kuwaasa watu kuchukua taadhari kabla hasa kwa kula na kunywa vitu asilia mfano matunda.
Ili kuwa na Afya daima na kuepuka maradhi unashauriwa kula matunda kila siku.

NJIA YA KUONDOA MAKOVU


Kuna matatizo malimbali ya ngozi yanayoweza kuwapata watu ambapo makovu ni mojawapo ya matatizo hayo.Makovu baadhi ya wakati hajawezi kuepukika hasa iwapo makovu hayo yamesababishwa na magonjwa au ajali mbalimbali. Makovu katika sehemu mbalimbali za mwili huweza kufunikwa na kufichwa kwa urahisi iwapo hayapo katika sehemu zinazoonekena. Lakini iwapo makovu yatakuwa usoni, mikononi au kifuani, huwa si rahisi kuyaficha na mara nyingi huwakera wale walio na makovu. Watu wengi wangependa kujua ni njia gani ambazo mtu anaweza kutumia ili kuondoa makovu. Ili kulijibu swali hilo ni bora kwanza tujue kovu ni nini hasa. Kovu katika mwili hutokea pale tishu aina ya fibrous inapojikusanya juu ya ngozi ili kusaidia kukarabati seli na ngozi iliyoharibika. Wakati kunapotokea jeraha, ngozi kutoa seli ziitwazo fibroblasts ambazo hutoa kitu kiitwacho collagen na kujaza sehemu yenye jeraha. Collagen ni ngumu, iko kama ufumwele unaopatikana katika protini ambayo hujaza eneo lote le kovu. Collagen ipo pia katika ngozi ya kawaida lakini katika kovu huwa nyingi na iliyojipanga katika mpangilio holela. Hii ndio sababu kovu huwa na rangi iliyokolea na huonekana kwa urahisi. Baadhi ya makovu huondoka kwa urahisi, baadhi huchukua miezi na hata miaka, huku makovu mengine yakibadilika polepole rangi na muonekano wake. Kovu huenekana kirahisi juu ya ngozi kwa sababu seli zilizotumika kuunda kovu hutofautiana na seli za mwanzo za ngozi. Kwa mfano makovu yaliyo juu ya ngozi hayawezi kuota vinyeleo kwa kuwa seli zake hazina matundu ya vinyeleo. Pia makovu hayana uwezo wa kuzuia miale ya jua. Kwa bahati mbaya ni vigumu kidogo kuweza kuondoa baadhi ya makovu moja kwa moja katika ngozi. Ingawa kuna njia kama vile vipodozi vinavyoweza kuziba makofu na njia nyinginezo za kitiba, lakina hata hivyo njia zote hizo mara nyingi huwa haziwezi kuondoa baadhi ya makovu kabisa, hasa yale makovu yaliozama katika ngozi na kuharibu kwa ngozi kwa kiasi kikubwa. Njia za tiba zinazoweza kutumiwa kuondoa makovu ni kama vile operesheni ya Laser (laser sugery), sindano za steroid, kubandua ngozi ya juu (dermabrasion) na radio therapy.
Lakini hata hivyo kuna njia mbalimbali za tiba asilia ambazo zinaaminika kuweza kusaidia kuondosha makovu. Njia hizo ni kama

1. Majani ya Aloe Vera. Majani haya yanapatikana kila sehemu hasa kwetu Tanzania na kwingineko Afrika. Majani hayo pia ni dawa nzuri ya kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi kama vile kiba au kishilingi. Kata majani hayo na utumie utomvu wake kupaka katika makovu. Baada ya muda polepole itapunguza na kuondoa makovu. Aleo Vera ni majani ambayo yanasifika hivi sasa ulimwenguni kote kwa ajili ya ngozi na yanatumiwa katika vipondozi mbalimbali. Basi zaidi ya kukuondoa makovu, yatasaidia pia kuifanya ngozi yako iwe nyororo.
2. Njia nyingine ni kutumia tango. Twanga tango na tumia mchanganyiko wake kupaka juu ya kovu. Husaidia kulainisha makovu na unapotumia kwa muda mrefu huondoa makovu pia.
3. Kupaka asali juu ya kovu na kuiacha usiku kucha. Njia hii inaweza kurudiwa mara kwa mara hadi pale kovu litakapotoweka.


5. Kupaka baking soda kidogo na maji sehemu yenye kovu na kuikanda sehemu hiyo kwa dakika moja. Mara mbili kwa siku. Kisha safisha kwa maji ya vuguvugu halafu paka mafuta ya zaituni.

6. Kutumia cream zenye vitamini E nad C na upake moja kwa moja katika kovu. Husaidia ngozi kuota tena katika kovu. Unaweza kumuona mtaalamu wa magonjwa ya ngozi naye akakushauri ni cream gani utumie ili kuondoa makovu yako. Pia jitahidi kupata lishe nzuri bila kusahau matunda na mboga mboga ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya ya ngozi. Kunywa maji ya kutosha kwani maji pia kulainisha ngozi yako na kufanya makovu kutoka kwa urahisi.

Inafaa kujua kuwa baadhi ya makovu kama vile yaliyosababishwa na kuungua au kuchanjwa ni vigumu kuyaondoa kwa kutumia njia hizo zilizotajwa.

JELI ITOKANAYO NA NYANYA

Utafiti mpya uliofanywa kwa majaribio umegundua kuwa katika mbegu za nyanya kuna mada asilia, inayoweza kusadia mzungumzo wa kawaida wa damu na kuzuia damu isigande. Mada hiyo iliyoko kwenye mbegu za nyanya iligunduliwa mwaka 1999 na Profesa Adim Dutta-Roy. Jeli hiyo inayozunguka mbegu za nyanya, hunaweza kusaidia mzunguko wa damu.
Jeli hiyo isiyokuwa na rangi wala ladha, huzuia chembe za damu aina ya platelets zisishikane, suala ambalo hupunguza uwezekano wa damu kuganda, kama inavyofanya aspirini lakini bila kuwa na madhara.
Wachunguzi wa Uingereza wamesema kwamba, athari za geli hiyo huanza masaa matatu tangu inapoanza kutumiwa na kudumu kwa masaa 18, hivyo inahitaji kutumiwa kila siku.
Wataalamu hao wamependekeza kwamba, kuongeza jeli hiyo katika vyakula mbalimbali kunaweza kuepusha matumizi ya aspirini kwa ajili ya kuzuia hatari ya magonjwa ya mishipa ya moyo.