
Sina shaka wengi wetu hatukuwa tunajua madhara yasababishwayo na unywaji wa soda kiburudisho kinachopendwa na wengi.Lakini leo kupitia blog hii ya grace kyasi utapata kujuzika juu ya madhara yatokanayo na unywaji wa kinywaji hiki aina ya soda pale tu inaponywewa zaidi ya mara moja kwa siku au mara kwa mara;
Kutokana na utafiti uliofanywa kwa kina na watafiti wa masuala ya vyakula na vinywaji nchini Marekani inaonesha kuwa Soda inauwezo mkubwa wa kuhatarisha figo za binadamu.Hatahivyo utafiti huo uliofanywa na watafiti kutoka chuo kikuu cha Harvard kilichopo nchini Marekani kwa zaidi ya wanawake 3000 nchini humo na kugundua kuwa unywaji wa soda unawaongezea hatari mara mbili ya kudhurika na figo.
Watafiti hao wameeleza kuwa matatizo hayo ya figo huweza kuwapata wanawake mara wanapokunywa soda zaidi ya mbili kwa siku,ambapo figo huanza kushuka utendaji kazi wake wa kawaida kitu ambacho kinaweza kusababisha madhara makubwa kiafya.Mbali na soda watafiti hao pia wamevituhumu vyakula vyenye sukari kuwa ndivyo husababisha matatizo ya Figo na kuwaasa watu kuchukua taadhari kabla hasa kwa kula na kunywa vitu asilia mfano matunda.
![]() |
Ili kuwa na Afya daima na kuepuka maradhi unashauriwa kula matunda kila siku. |
0 comments:
Post a Comment